About CHF

CHF iliyoboreshwa ni bima ya afya kwa ajili ya wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro na Manyara ambao hawana uwezo au hawajatimiza vigezo vya kujiunga na bima ya afya ya taifa (NHIF). Bima hii inaendeshwa na mfuko wa bima ya taifa (NHIF) kupitia ofisi za kwenye mikoa husika kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la PharmAccess. Halmashauri zote ndani ya mkoa ndio wasimamizi wa CHF iliyoboreshwa.
CHF iliyoboreshwa imeanzishwa kuondoa changamoto zilizokuwepo kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF) ulioanzishwa mwaka 2001. Katika CHF iliyoboreshwa, huduma zinatolewa katika hospitali na zahanati za binafsi, mashirika ya dini na zile za serikali.
Gharama ya kujiunga ni shilingi elfu thelasini (Tsh. 30,000) kwa kaya (mwanachama, mwenza wake na Watoto wanne) kwa ajili ya huduma kwa mwaka mmoja.
Mpango huu ni wa kudumu, kwa kuwa NHIF wamedhamiria kuuendesha wenyewe na hata baadaye kuupeleka kwenye mikoa mingine.

No comments:

Post a Comment