Friday, 16 December 2016

Kukabidhi pikipiki wa iCHF officers

Naibu waziri wa afya Mh. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya pikipiki zinazotumiwa na maofisa wa iCHF kufikia wananchi.

Wednesday, 23 November 2016

Huduma nzuri kwa wateja wa iCHF yahimizwa

Rombo, August 2016

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bw Lembris Kipuyo amewahimiza watoa huduma wote kuhakikisha kuwa wanahudumia wanachama wa CHF iliyoboreshwa bila kuwabagua kwani wao walishalipia huduma kabla hata hawajaugua. “

Ninafahamu kuta watoa huduma huwa wanawabagua wanachama wa CHF, sasa natoa onyo kwa yoyote atakayefanya hivyo tutamchukulia hatua kali za kisheria.” alisema huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa uhamasishaji wa CHF iliyoboreshwa.

Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kusimamia hilo na kuhakikisha malalamiko halo hayatokei tena. “ Hawa walishalipia huduma zao kabla hawajaugua lakini pia kwenye maboresho vituo vinalipwa fedha zao mwanzo wa mwezi hivyo hakuna sababu ya kuwabagua au kuwanyima huduma na dawa”. Mkuu huyo wa Wilaya pia amewahimiza wananchi wachangamkie fursa ya kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya kwa gharama nafuu kwa mwaka mzima kwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (iCHF) embat kwa sasa watapata huduma kwenye vituo vya serikali na vya taasisi za kidini wilayani humo ikiwemo Hospitali ya Ngoyoni ambayo avaló hawakuweza kupata huduma hapo.

Naibu Waziri azindua CHF iliyoboreshwa wilaya ya Babati

Naibu  Waziri wa Afya, Mh. Hamisi Kigwangalla (MB) amezindua CHF iliyoboreshwa mkoani
Manyara, wilaya ya Babati huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa vituo vyote vya huduma za afya, zikiwemo zile za dini zinatoa huduma bora zisizo na ubaguzi kwa wanachama wote waliojiunga.

Katika hotuba yake ya dakika 45, Mh. Naibu Waziri alisema kuwa anafahamu kuna hospitali moja ya dini iliyoko mkoani humo ambayo licha ya kupokea ruzuku serikalini na kupata malipo toka katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa, lakini bado wananyanyasa wateja wa CHFiliyoboreshwa (iCHF). “Nichukue nafasi hii kuwaonya baadhi watumishi wa taasisi za serikali, ambao tunafahamu huwa wanatabia ya kuwahudumia vibaya wanachama wa CHF kwa makusudi ili wasijiunge, waache mara moja! Kwa kutumia simu ya bure, wananchi muwafichue ili tuwashughulikie ipasavyo”, alisema Naibu Waziri.

Katika hotuba yake iliyokuwa ikikatishwa na makofi na vigelegele toka kwa wananchi, Naibu Waziri pia aligusia suala la upatikanaji wa dawa, huku akiwataka daktari wa mkoa na madaktari wa wilaya kusimamia vituo vya huduma za afya ndani ya maeneo yao kuhakikisha dawa zinakuwepo wakati wote.
Mheshimiwa Naibu Waziri pia aligusia suala la afya za vijana, hasa waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakipata ajali mara nyingi huku wakishindwa kugharamia huduma za afya kwa kuwataka wawekewe utaratibu utakaowalazimisha wale wamiliki wa pikipiki kuwalipia bima ya iCHF madereva wa bodaboda.

Kabla ya uzinduzi huo, Naibu Waziri alitembelea kituo cha afya cha Dongobesh, kilichopo wilayani Mbulu ambako alikata utepe kukizindua kufuatia ukarabati mkubwa uluofanywa kwa ufadhili wa PharmAccess International na pia kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa chumba cha upasuaji kinachojengwa kwa nguvu ya wananchi na fedha za halmashauri.