Rombo, August 2016
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bw Lembris Kipuyo amewahimiza watoa huduma wote kuhakikisha kuwa wanahudumia wanachama wa CHF iliyoboreshwa bila kuwabagua kwani wao walishalipia huduma kabla hata hawajaugua. “
Ninafahamu kuta watoa huduma huwa wanawabagua wanachama wa CHF, sasa natoa onyo kwa yoyote atakayefanya hivyo tutamchukulia hatua kali za kisheria.” alisema huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa uhamasishaji wa CHF iliyoboreshwa.
Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kusimamia hilo na kuhakikisha malalamiko halo hayatokei tena. “ Hawa walishalipia huduma zao kabla hawajaugua lakini pia kwenye maboresho vituo vinalipwa fedha zao mwanzo wa mwezi hivyo hakuna sababu ya kuwabagua au kuwanyima huduma na dawa”. Mkuu huyo wa Wilaya pia amewahimiza wananchi wachangamkie fursa ya kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya kwa gharama nafuu kwa mwaka mzima kwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (iCHF) embat kwa sasa watapata huduma kwenye vituo vya serikali na vya taasisi za kidini wilayani humo ikiwemo Hospitali ya Ngoyoni ambayo avaló hawakuweza kupata huduma hapo.
No comments:
Post a Comment